Muda wa kubaki Swafaa na Marwah

765- Ahmad ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa az-Zubayr bin ´Adiy, kutoka kwa Ibraahiym ambaye amesema:

“Ubakiaji wa Swafaa na Marwah unatakiwa kuwa mrefu sawa na Suurah an-Najm.”

766- Ahmad ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Abu Waa-il, kutoka kwa Ibn Mas´uud aliyesema wakati alipokuwa akitembea kati ya Swafaa na Marwah:

رب اغفر و ارحم، إنك أنت الأعز الأكرم

“Mola nisamehe na unirehemu! Kwani hakika Wewe ndiye mtukufu, mkarimu zaidi.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 161
  • Imechapishwa: 26/03/2021