Muda mrefu wa nifasi kwa mtazamo wa Ibn ´Uthaymiyn

Wanachuoni wa Hanaabilah wanasema ya kwamba muda mrefu wa nifasi ni siku arubaini.

Kuna rai nyingine katika suala hili inayosema kwamba ni siku sitini. Hii ni rai ya ash-Shaafi´iy. Shaafi´iyyah wanasema kuwa kuna wanawake wengi ambao nifasi zao zinaendelea kwa siku sitini. Kwa hiyo si jambo la nadra ili tuseme kuwa jambo hili linakosa hukumu.

Mimi naonelea kuwa rai hii ndio sahihi, kwamba nifasi inaweza kuwa kwa siku sitini kwa sharti iwe ni damu ileile inayotoka. Shaykh-ul-Islam (Rahimahu Allaah) amesema kwenye “al-Ikhtiyaaraat” ya kwamba nifasi inaweza kuwa kwa siku sitini sabini maadamu ni damu ileile isiyobadili sura yake, harufu au kitu kingine. Ingawa nifasi inaweza kuwa kwa siku sabini, mimi nasema itaendelea kwa siku sitini. Huenda hii ndio rai sahihi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath Dhiyl-Jalaal wal-Ikraam (1/738)
  • Imechapishwa: 24/09/2020