Muasi mume wako!


Swali: Mume wangu ananitaka niondoshe nyusi kwa sababu ni jambo linampendeza…

Jibu: Hapana, usimtii. Ni wajibu kwako kumuasi. Mume huyu ni mtenda dhambi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwanamke mwenye kuwanyoa wenzao nyusi na yule mwenye kunyolewa; halafu huyu anamwamrisha kunyoa nyusi zake? Hiki ni kitendo cha jinai. Huu sio wanaume.

Swali: Ni zipi nasaha zako kwa baadhi ya waume ambao wamepewa mtihani wa kuwaangalia wanawake kwenye TV kisha baada ya hapo wanapenda wake zao wawe na sifa kama za wale wanawake?

Jibu: Wasitiiwe:

”Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Ni wajibu kwa mume huyu kutubu kwa Allaah, ateremshe macho yake na asitazame TV zinazofitinisha na maono mabaya. Atafanyiwa hesabu mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ipo siku miongoni mwa siku zake ambapo hatopata kumkimbia Allaah (´Azza wa Jall). Ni wajibu kwake kutubu kwa Allaah na aachane na mambo haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (49) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/m-3%20%20-%2012%20-%202%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/10/2018