Mtumzima ametoa fidia ya pesa kabla ya kuingia Ramadhaan

Swali: Kuna mtu hawezi kufunga na anaumwa ugonjwa ambao hautarajiwi kupona. Mwaka huu ametoa fidia pesa kabla ya kuingia mwezi wa Ramadhaan. Je, kitendo chake ni sahihi? Ikiwa si sahihi afanye nini sasa?

Jibu: Hizo pesa alizotoa kabla ya Ramadhaan zinazingatiwa swadaqah. Atapewa thawabu – Allaah akitaka. Lakini hata hivyo hazisihi badala ya swawm kutokana na sababu mbili:

Ya kwanza: Hakuzitoa katika muda wa swawm.

Ya pili: Ametoa pesa.

Fidia ni lazima iwe chakula kuwapa masikini kama alivyosema Allaah (´Azza wa Jall):

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ

”… kwa wale wanaoiweza lakini kwa tabu watoe fidia kuwalisha masikini.”[1]

Kwa hivyo tunamwambia ndugu huyu ambaye alitoa pesa kabla ya kuingia Ramadhaan kwamba ni swadaqah. Hivi sasa anatakiwa kulisha masikini 29. Ima anaweza kuwakusanya katika chakula cha mchana au cha jioni. Kwa mfano wanaweza kuja siku mbalimbali. Kwa mfano siku ya kwanza unaweza kufanya chakula cha mchana au cha jioni cha masikini tano. Siku ya pili ukafanya chakula cha watu tano. Siku ya tatu mpaka ukawakamilisha. Ni sawa. Vinginevyo unaweza kutoa kitu kingine mbali na chakula kama vile nafaka. Kiwango chake ni 1 kg ya mchele. Hapo itakuwa imetakasika dhimma yako.

[1] 02:184

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/917
  • Imechapishwa: 04/05/2018