Swali: Neno “muweka Shari´ah”, Musharriy´, inajuzu kumwita nalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au ni maalum kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa)?

Jibu: Asli ya mwekaji Shari´ah ni Allaah (Jalla wa ´Alaa). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mfikishaji kutoka kwa Allaah. Ni mwekaji Shari´ah bi maana ni mfikishaji kutoka kwa Allaah yale Aliyoyaweka. Haina neno kumwita hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_15.mp3
  • Imechapishwa: 14/06/2018