Mtume haombwi uombezi baada ya kufa

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuomba uombezi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada kufa kwake?

Jibu: Maiti haombwi kitu, sawa ikiwa ni uombezi au kitu kingine[1]. Maswahabah hawakuwa wanaenda kwenye kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumuomba du´aa, uombezi au msamaha. Wao ni wajuzi zaidi katika Ummah juu ya yanayojuzu na yasiyojuzu kwa kuwa wao ni wanafunzi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lau wangelijua kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa jambo hili linajuzu wangelifanya. Kile kitendo chao cha wao kuacha ni kwamba walijua kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa kitendo hichi hakijuzu na hakifanywi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kumuomba-maiti-msamaha-baada-ya-kufa/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-1-30.mp3
  • Imechapishwa: 09/08/2020