Mtume amesema kuwa sio halali vipi wewe useme kuwa ni halali?


Swali: Ni lipi jibu kwa mwenye kusema kwamba inajuzu kwa mwanamke kusafiri pasina kuwa na Mahram ikiwa ni safari fupi na kunaaminika usalama?

Jibu: Jibu ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Sio halali…”

Anasema sio halali. Mtume anasema kuwa sio halali. Vipi sisi tuseme kuwa ni halali?

“Sio halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Hakuna nafasi ya maneno ya yeyote baada ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-01-27.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014