Mtume Amekingwa Kwa Hali Yoyote


Swali: Ni ipi hukumu kwa ambaye anapinga kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakukingwa na kukosea?

Jibu: Akiwa ni mjinga au ni mfuata kichwa mchunga ni mpotevu. Ama akiwa ni mwenye kukusudia ni kafiri. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekingwa na kukosea. Amekingwa kwa hali yoyote hata kama atapitikiwa na baadhi ya mambo yenye kutokamana na Ijtihaad zake ambazo mwishoni amekingwa na kukosea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bi maana haachwi kwenye kosa kwa hali yoyote ile.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2053
  • Imechapishwa: 31/01/2017