Mtume amekhusika na fadhilah za kumswalia

Swali: Allaah kumsifu mara kumi yule ambaye anamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo maalum kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au inajumuisha Mitume wengine?

Jibu: Imepokelewa katika Hadiyth ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah amenipa kwa ambaye ananiswalia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mara kumi.”

Udhahiri wake ni kwamba ni kitu maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu Mitume wengine Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 22/10/2021