Swali: Baadhi ya ambao wanapinga sifa za Allaah wanaeneza utata juu ya sifa ya Allaah kuwa juu. Moja katika shubuha hizo ni kwamba haijuzu kuuliza Allaah yuko wapi kwa sababu ni swali ambalo linaulizwa juu ya mahali. Ni upi usahihi wa hili?

Jibu: Ina maana ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa mpotevu pindi alipomuuliza mjakazi:

“Allaah yuko wapi?”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuuliza: “Allaah yuko wapi?” Akajibu: “Mbinguni.” Ndipo akasema: “Mimi ni nani?” Akajibu: “Mtume wa Allaah.” Ndipo akasema: “Mwache huru, kwani hakika ni muumini.”[1]

Ina maana ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikosea wakati alipouliza swali hili. Allaah (Subhaanah) yuko mbinguni, juu, amelingana juu ya ´Arshi, kama alivyosema Mwenyewe. Kwa mtazamo wa mtu huyu kwa mujibu wa ´Aqiydah yake anaonelea kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikosea? Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ

“Je, mnadhani mko katika amani na Aliyeko mbinguni kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?” (67:16)

Anajizungumzia Yeye Mwenyewe. Allaah (Subhaanah) yuko mbinguni, juu, juu ya mbingu, amelingana juu ya ´Arshi Yake. Vinginevyo atakuwa wapi? Atakuwa amechanganyika na viumbe Vyake? Hii ni kufuru. Mwenye kuonelea kuwa Allaah amekita na kuchanganyika na ulimwengu Wake ni kafiri kwa sababu hakumtakasa Allaah na kuchanganyika na watu sehemu chafu, vyoo na taka. Anasema kuwa Allaah yuko kila mahali?

[1] Muslim (537).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-10-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020