Swali: Je, Israa´ na Mi´raaj ilikuwa katika hali ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa macho au hapana? Je, Mtume alimuona Mola Wake kwa macho yake?

Jibu: Israa´ na Mi´raaj ilipitika hali ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yuko macho, kama ilivyokuja katika dalili za Kishari´ah. Hakumuona (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa macho yake. Hii ndio jopo la wengi katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (266-267/03)
  • Imechapishwa: 23/08/2020