Mtume (´alayhis-Salaam) Alikuwa Hajui Kusoma Alifunzwa Na Allaah


Swali: Kumeenea kisa kinachosema ya kwamba haijuzu kumsifu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa alikuwa hajui kusoma na kwamba alikuwa anajua kuandika na kusoma. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Huu ni uongo. Huu ni uongo na ni ujinga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam alikuwa hajui kusoma wala kuandika:

وَمَا كُنتَ تَتْلُو مِن قَبْلِهِ مِن كِتَابٍ وَلَا تَخُطُّهُ بِيَمِينِكَ

“Na wala hukuwa ukisoma kabla yake [Qur-aan] kitabu chochote na wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume.” (29:48)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipokuwa anataka kuandika kitu, anaita mwandishi. Pindi Qur-aan inaposhushwa anaita mwandishi ili aandike. Alikuwa hajui kuandika kabisa. Alikuwa hajui kusoma wala kuandika. Pamoja na hivyo Allaah Akamteremshia Qur-aan hii ambayo ni miujiza. (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa hajui kusoma wala kuandika, lakini Allaah Akamfunza na Akamteremshia Qur-aan. Alikujuwa si msomi kwa njia ya kwamba alikuwa hajui kusoma wala kuandika. Ama inapokuja katika elimu, Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Alimfunza elimu ambayo mwingine hakupata:

وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمْ تَكُن تَعْلَمُ ۚ وَكَانَ فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ عَظِيمًا

“Na Allaah Amekuteremshia Kitabu na Hikmah na Akakufunza yale ambayo hukuwa unayajua. Na fadhila za Allaah juu yako ni kuu.” (04:113)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf--02041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2015