Mtume akiwa mwafrika na mfupi ndotoni – kweli ndiye?


Swali: Mwenye kumuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usingizini akiwa mfupi au mweusi. Vipi hilo litawezekana ilihali Hadiyth inasema:

“Atakayeniona basi ameniona kweli. Kwani hakika shaytwaan hawezi kujifananisha na mimi.”?

Jibu: “Atakayeniona… “

bi maana atakayemuona katika maumbile yake yaliyothibiti katika Hadiyth. Haina maana yule atakayemuona katika maumbile yanayoenda kinyume. Yule atakayemuona katika maumbile yanayoenda kinyume basi huyo siye.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 26/03/2018