Mtu wa kijani anayeleta baraka

Swali: Mimi namwamini Allaah asiyekuwa na mshirika. Lakini nimesikia kuwa kuna bwana mmoja ni mwenye nguo nyeupe pee na haonekani kuwa na alama ya safari. Mtu huyu anaitwa “mtu wa kijani”. Bwana huyu anapokupa kitu basi inazidi baraka ya mali yako. Anaposhuka kwenye duka basi faida yake inaongezeka. Je, mambo haya yanaingia akili au ni katika Bid´ah?

Jibu: Maneno haya ni batili na hayana msingi wowote. Mtu huyu hakuna uwepo wake. Baadhi ya watu wanadai kuwa al-Khidhr ndiye mlengwa, kitu ambacho hakina usahihi. al-Khidhr alikufa kabla ya kutumilizwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanachuoni. Ukhurafi huu uliotaja wote ni katika uzushi wa shaytwaan usiokuwa na msingi wowote. Unatakiwa kutambua hivo na wala usighurike na maneno ya waganga hawa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/486)
  • Imechapishwa: 08/03/2021