Mtu Wa Dini Hawezi Kusimama Nyuma Ya Ugaidi


Swali: Sisi na kila mtu ambaye yuko macho ameudhika na ulipuaji, kama ulivyotanabahisha hilo katika Khutbah na maelezo ya kamati ya Kibaar-ul-´Ulamaa. Hata hivyo jambo ambalo limetuudhi zaidi ni magazeti na vyombo vya khabari kuwahujumu watu wa Dini. Ni ipi nasaha yako kwa mambo haya?

Jibu: Ni kitu kilichokuwa kinasubiriwa kwa watu waovu na waharibifu kuhujumu baada ya ajali hii. Watu wanachongoja ni kupatikane fursa ili waweze kusema lile wanalolitaka. Hili ni katika madhara ya malipuaji haya. Miongoni mwa madhara yake ni kuwa watu wanawatia watu wote wa Dini katika mkumbo mmoja. Pamoja na kuwa tunajua kwamba mtu mwenye Dini kabisa hawezi kufanya matendo kama haya machafu na watu wa Dini kabisa wanajiweka mbali na matendo haya na wanayakataza kwa mioyo yao na midomo yao. Lakini watu wa shari wanatumia kila fursa na kuzungumza vile wanavyotaka. Allaah (Ta´ala) Amesema katika Kitabu Chake:

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ ۖ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ

“Na kwa yakini Tumemuumba mwanaadamu na Tunajua yale (yote) yanayomshawishi nafsi yake, na Sisi Tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingo (yake). Pale wanapopokea wapokeaji (Malaika wanaodhibiti ‘amali) wawili wanaokaa kuliani na kushotoni.” (50:16-18)

Hata hivyo kuna jambo lingine. Kuna baadhi ya ´Awwaam wajinga ambao wanakimbiza watu katika kuwa na msimamo na kuwa mtu wa Dini na wanasema:

“Tazama wale wenye misimamo na wenye Dini wanayoyafanya!”

Hili ni kosa. Watu hawa ambao wamefanya matendo haya sio Dini yao ndio imewaongoza katika hayo. Lau hakika wangelirejea katika Qur-aan na Sunnah, wangelijua kihakika kwamba kitendo hichi ni haramu na sio Dini inayomkurubisha mtu kwa Allaah. Uhakika wa mambo ni kwamba ni uadui dhidi ya waja wa Allaah (´Azza wa Jall). Kwa ajili hiyo haifai kwa ´Awwaam kutumia hili kuwa ni fursa ya kutahadharisha watoto wao kuwa na msimamo wa Dini uliyojengwa juu ya mfumo sahihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36)
  • Imechapishwa: 23/04/2015