Mtu mwenye kunukia vibaya msikitini


Swali: Je, mtu ambaye ananukia vibaya anaacha kuswali swalah ya mkusanyiko?

Jibu: Ikiwa anawaudhi wale walio pembeni yake, aache kuswali swalah ya mkusanyiko. Badala yake aswali nyumbani kwake. Kadhalika ambaye amekula kitunguu saumu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemkataza mtu kama huyu kuingia msikitini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (87) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-3-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 17/11/2018