Swali: Akiingia mtu msikitini na safu imejaa nyuma ya imamu na wala hakurudi nyuma yeyote katika safu, je aswali peke yake?

Jibu: Ajipenyeze katika ile safu na aswali. Na ikiwa hakupata nafasi kabisa aswali upande wa kulia wa imamu akiweza. Asiswali peke yake katika safu. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Hana swalah kwa mwenye kuswali peke yake katika safu.”

Ni juu ya aliyeingia asubiri ikiwa hakupata nafasi [kwa ile safu]. Akipata mtu wakuswali naye himdi zote anastahiki Allaah, la sivyo ataswali peke yake baada ya swalah imamu kutoa salamu. Mara nyingi mtu hujitahidi kujipenyeza katika safu na hupata fursa hata ikiwa katikati ya safu mpaka aswali katika safu. Lakini ikiwa hakupata kitu na hakuweza kuswali pembezoni mwa upande wa kulia kwa imamu, atasubiri aswali peke yake baada ya imamu au akaja mtu wakaswali nae katika safu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=BCzEMyKvdFg
  • Imechapishwa: 10/04/2022