Mtu kurudi katika mji aliouacha kwa ajili ya Allaah ili kutafuta kazi


Swali: Kuna mtu mmoja mfaransa amesilimu, kisha akasafiri kwenda Yemen na kuoa. Lakini ametafuta kazi na hakupata. Kisha akasafiri kwenda Ufaransa kutafuta kazi. Je, anapata kurudi katika mji wake?

Jibu: Muislamu akihama kutoka katika mji asirudi. Kwa ajili hiyo ndio maana Muhaajiruun hawakurudi Makkah pamoja na kuwa Makkah ndio mahala bora kabisa. Lakini pamoja na hivyo hawakurudi baada ya Makkah kutekwa na waislamu. Hata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakurudi baada ya kutekwa kwa kuwa ameuacha kwa ajili ya Allaah. Mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Allaah hakirudilii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (52) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-06-05.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014