Mtu kunuia Tahiyyat-ul-Masjid na mkusanyiko unaoswali faradhi

Swali: Inajuzu kwa muislamu kujiunga na swalah ya faradhi na huku ananuia Tahiyyat-ul-Masjid? Kwa mfano nimejiunga na wewe katika msikiti huu ilihali nimeshaswali kabla yenu inafaa kwangu kunuia kuwa ni Tahiyyat-ul-Masjid?

Jibu: Mtu akiingia msikitini na akaswali swalah ya faradhi inamtosheleza kutokamana na Tahiyyat-ul-Masjid. Hakuna haja ya kunuia Tahiyyat-ul-Masjid. Malengo ya Tahiyyat-ul-Masjid ni wewe usikae isipokuwa umeswali Rak´ah mbili hizi. Jambo hili linapatikana kwa kuswali swalah hii ya faradhi na Raatibah ya kabla ya swalah. Ikiwa utaingia msikitini baada ya adhaana ya Fajr na wewe hujaswali Rak´ah mbili za Raatibah na ukawa umeziswali wakati ulipoingia zinatosheleza kutokamana na Tahiyyat-ul-Masjid. Vivyo hivyo iwapo utaingia na ukawakuta watu wanaswali ambapo ukajiunga nao inakutosheleza kutokamana na kuswali Tahiyyat-ul-Masjid. Kujiunga na watu walio wanaswali ni sunnah, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anawakhutubia wanaume wawili:

“Mtaposwali majumbani mwenu kisha mkaja msikitini mkakuta watu wanaswali mkusanyiko, swalini pamoja nao. Hakika kwenu itakuwa ni sunnah.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (31) http://binothaimeen.net/content/704
  • Imechapishwa: 03/11/2017