al-Fawzaan mgonjwa kulipa zwalah zilizompita alipokuwa amelala kwenye koma

Swali: Ni yapi maoni yenye nguvu kuhusiana na mtu aliyelala kwenye koma zaidi ya siku tatu? Ni lazima kwake kulipa swalah zilizompita katika kipindi hicho?

Jibu: Ni rahisi kulipa [swalah za] siku tatu. Swalah zilizompita pindi amelala kwenye koma masiku mengi au miezi asizilipe. Ama ikiwa alilala kwenye koma siku tatu au chini ya hapo azilipe. Ni sahali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Imechapishwa: 26/10/2016