Mtu kula kutoka kwenye kichinjwa alichokiwekea nadhiri

Swali: Nilimuwekea Allaah (Ta´ala) nadhiri ya kuchinja na nikaitimiza nadhiri yangu ambapo nilichija. Lakini hata hivyo nilikula mimi na familia yangu kutoka kwenye kichinjwa hicho. Nimesikia kuwa haijuzu kula kutoka kwenye kichinjwa hicho. Ni kipi kinachonilazimu? Nirudi kuchinja kwa mara nyingine au nitoe pesa kiwango nilichokula mimi na familia yangu ambapo inaweza kufikia nyama takriban 3 kg?

Jibu: Nadhiri na kuchinja ni mambo yamegawanyika sampuli mbili:

1 – Kujikurubisha kwa Allaah ambapo mtu anachinja kwa nia ya kujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall). Kuchinjwa hichi asile. Anachotakiwa ni yeye kuitoa swadaqah kwa mafukara.

2 – Nadhiri ya kuchinjwa iwe ni mazowea na si ´ibaadah. Kwa msemo mwingine mtu akusudie kufurahi, watu wakusanyike kwake na mambo mengine yaliyoruhusiwa. Nadhiri aina hii haina hukumu ya ´ibaadah. Ni nadhiri iliyoruhusiwa [mubaah]. Mtu akitaka kuitimiza atafanya hivo na akitaka atatoa kafara ya yamini au asitimize. Kigawanyo hichi akitimiza kile alichokiwekea nadhiri basi inafaa kwake kula kutoka kwenye kichinjwa hicho yeye na familia yake. Hakuna neno kwake juu ya hilo. Ama aina ya kwanza ambayo amekusudia kujikurubisha kwa Allaah (Ta´ala), tumekwishasema kuwa anatakiwa kuitoa swadaqah kuwapa mafukara. Kama alikula kutoka kwenye kichinjwa hicho basi atoe pesa kiwango alichokula na awape mafukara.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (18) http://binothaimeen.net/content/6828
  • Imechapishwa: 13/09/2021