Mtu huyu anaweza kuwa ni al-Khadhir?


Swali: Mimi namwamini Allaah kuwa ni Mmoja asiyekuwa na mshirika, lakini nimesikia watu wakisema kuwa kuna mtu mwenye mavazi meupe sana na hakuonekani kwake athari za safari. Mtu huyu akikupa kitu, basi baraka ya mali yako inazidi. Naomba faida, je, mambo haya yanaingia akilini au ni katika Bid´ah?

Jibu: Kauli hii ni ya batili na haina msingi wowote. Na mtu kama huyu hapatikani. Na baadhi ya watu wanadhani kuwa aliyekusudiwa hapa ni al-Khadhir, na hili ni jambo lisilokuwa na usahihi wowote. al-Khadhir alikufa muda tu kabla ya kuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni. Na ukhurafi huu uliyosema, ni katika mambo ya Kishaytwaan na hayana msingi wowote. Inatakikana ujue hilo, na usidanganyike na maneno ya watu hawa wachawi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 18/03/2018