Mtu hupendwa na Allaah kwa kujibidisha na Sunnah  

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

38- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

“… na mja Wangu hatoacha kujikurubisha Kwangu kwa vitendo vya Nawaafil mpaka mwishowe nije kumpenda.”

Bi maana atakithirisha kuleta ´ibaadah nyingi za Nawaafil, ikiwa ni pamoja na swalah na Nawaafil, swawm, swadaqah, Hajj, ´Umrah na mfano wa hayo.

“… mpaka mwishowe nije kumpenda.”

Hii ni dalili inayoonyesha ya kwamba mapenzi ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) yanapatikana kwa kufanya bidii ya kumuabudu kwa kutekeleza ´ibaadah za Nawaafil. Hili linakuwa baada ya kutekeleza mambo ya faradhi na kujikurubisha kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwayo.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 511
  • Imechapishwa: 10/05/2020