Mtu hawezi kuburudika kwa riziki pamoja na khofu

Swali: Katika Suurah “al-Baqarah” na “Ibraahiym” ametaja amani kabla ya riziki. Una la kusema juu ya hilo?

Jibu: Ndio. Mtu hawezi kuburudika kwa riziki pamoja na khofu. Riziki inaburudikiwa pamoja na amani. Kwa ajili hiyo ndio maana Ametaja kwanza amani kabla ya riziki:

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ

“Na [taja] aliposema Ibraahiym: “Mola wangu Ufanye mji huu kuwa wa amani na Waruzuku watu wake katika matunda atakayemwamini Allaah miongoni mwao na Siku ya Mwisho.” (02:126)

Ibraahiym (´alayhis-Salaam) aliomba kwanza amani kisha ndio akaomba riziki. Kwa kuwa hakuna kuburudika kwa riziki pasi na amani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 06/06/2018