Swali: Inajuzu kwa Muislamu kunuia nia mbili kwa wakati mmoja? Kama kwa mfano kunuia Swalah iwe ya Sunnah ikiwa atakosea katika Swalah ya faradhi, au akakosea katika Hajj au Zakaah?

Jibu: Hatujui kuwa hili lina asli. Bali asli ni salama na afya. Anuie Swalah anayoswali kama anavyotaka; Sunnah ya Dhuhr, Sunnah ya Maghrib, Sunnah ya ´Ishaa, Sunnah ya Dhuhaa bila ya kuwa na mashaka (wasiwasi) aliyoashiria. Asli ni salama. Alhamdulillaah. Na wala hatujui kuwa hili lina asli yoyote ya kuweka nia mbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 18/03/2018