Mtu anaweza kufanya I´tikaaf katika mwezi mwingine mbali na Ramadhaan?

Swali: Kufanya I´tikaaf nje ya Ramadhaan ni jambo limewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Lililowekwa katika Shari´ah ni kukaa I´tikaaf katika Ramadhaan peke yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufanya I´tikaaf kwa isiyokuwa Ramadhaan mbali na Shawwaal. Sababu ilikuwa kwamba Ramadhaan moja wapo aliacha kufanya I´tikaaf ndipo akawa amefanya katika Shawwaal. Lakini endapo mtu atafanya I´tikaaf katika mwezi mwingine mbali na Ramadhaan itakuwa ni jambo lenye kujuzu. Kwa sababu ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema:

“Mimi niliweka nadhiri kukaa I´tikaaf usiku au mchana katika msikiti Mtakatifu.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Tekeleza nadhiri yako.”

Lakini hata hivyo mtu hakuamrishwa na wala haikupendekezwa kwake kufanya I´tikaaf katika mwezi mwingine usiokuwa Ramadhaan.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/159-160)
  • Imechapishwa: 15/06/2017