Mtu anatakiwa kukataza maovu kwa hali yoyote ile


Swali: Maasi yamekuwa mengi hii leo na ni wachache wanaokataza. Ni lipi la wajibu kwa waislamu juu ya hayo?

Jibu: Lililo la wajibu ni kukataza kadiri na uwezo, kama alivyosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu basi ayakataze kwa mkono wake, asipoweza afanye hivo kwa mdomo wake, asipoweza afanye kwa kuchukia – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”[1]

Mtu akataze maovu kwa kiasi cha uwezo. Asikubalieni na maovu kabisa. Akataze maovu kwa kiasi cha uwezo wake; ima kwa kutumia mkono, mdomo au kwa kuchukia. Hii ndio ngazi ya mwisho. Asiridhie maovu na akakubaliana na maovu. Akataze maovu japokuwa kwa moyo wake. Atapokataza kwa moyo wake anatakiwa vilevile kujiepusha na wenye kufanya hivo na sehemu hiyo.

[1] Ahmad (3/10) na Muslim (49).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (83) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-15-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/01/2018