Mtu anatakiwa ajipambe siku ya ´Iyd


Swali: Ni yepi maoni yako kuhusu yale yanayosemwa na baadhi ya wanachuoni kwamba yule mwenye kufanya I´tikaaf anatakiwa kutoka kwenda katika ´Iyd akiwa na mavazi ya I´tikaaf yake?

Jibu: Naona kuwa jambo hili linaenda kinyume na Sunnah. Sunnah siku ya ´Iyd ni mtu ajipambe. Ni mamoja akiwa ni mwenye kufanya I´tikaaf au si mwenye kufanya I´tikaaf.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/236)
  • Imechapishwa: 14/06/2018