Mtu anapoenda katika Sujuud atangulize mikono au magoti kwanza?

Swali 29: Mtu anapoenda katika Sujuud atangulize mikono au magoti kwanza?

Jibu: Atangulize magoti. Hivi ndio bora. Hii ndio Sunnah. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pindi mmoja wenu anaposujudu basi asende chini kama anavoenda chini ngamia.”

Ngamia hutanguliza kwanza mikono yake/miguu yake ya mbele. Isipokuwa ikiwa kama hawezi, kama mimi hivi na mfano wangu, ndipo atangulize mikono yake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 36
  • Imechapishwa: 05/11/2018