Mtu anafanya nini akiwa na pesa za madawa ya kulevya asizozitaka?

Swali: Kuna mtu yuko na pesa aliyoihifadhi inayotokana na madawa ya kulevya. Azifanyishe nini pesa hizo baada ya kutubia?

Jibu: Atajikwamua nazo kwa kuzigawa kwa watu wahitaji. Hata hivyo anafanya hivo kwa lengo la kujinasua na si kwa lengo la kutoa swadaqah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (29)
  • Imechapishwa: 11/02/2022