Mtu amewahi Rak´ah akimkuta imamu katika Qunuut baada ya Rukuu´?

Swali: Kuna mtu aliingia msikitini akamkuta imamu yuko katika Qunuut ambapo akasema “Allaahu Akbar”, akaenda katika Rukuu´ na kuinuka kutoka katika Rukuu´ kisha akanyanyua mikono yake na kuanza kukunuti pamoja na imamu na kutoa Salaam pamoja naye. Je, inasihi kufanya hivo?

Jibu: Kitendo hichi si sahihi. Huku sio kumuabudu Allaah kwa njia kama hii mtu akamuabudu kwa Rak´ah aliyoiwahi katika Qunuut. Kwa sababu ili kuiwahi Rak´ah ni lazima uiwahi katika hali ya kusimama, kurukuu, kusujudu na kukaa. Mtu huyu hakurukuu na wala hakusimama kabla ya kurukuu pamoja na imamu. Alichofanya ni yeye kusimama baada ya kurukuu. Tunasema kuwa kitendo kama hichi hakijuzu. Huku ni kuzifanyia shere Aayah za Allaah. Imamu wake atapoleta Tasliym basi ni lazima kwake kuswali Rak´ah hiyo ambayo imempita.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/129)
  • Imechapishwa: 17/06/2017