Swali: Mtu ambaye aliacha swalah nyingi kisha akatubu azilipe au hapana?

Jibu: Kwa mujibu wa maoni sahihi asizilipe. Inatosheleza kwake kutubu tawbah ya kweli na kuendelea kuhifadhi swalah. Wenye kusema kuwa anatakiwa kuzilipa ni wale wenye kuonelea kuwa hakufuru. Wanasema kuwa mwenye kuacha swalah hakufuru bali ni mtenda maasi. Hawa ndio wenye kusema kuwa azilipe.

Kuhusiana na wenye kusema kuwa mwenye kufanya hivo anakufuru kufuru kubwa, wanasema kuwa atubu kwa Allaah na kuingia katika Uislamu upya. Haya ndio maoni sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-13.mp3
  • Imechapishwa: 09/06/2018