Mtu akiswali na imamu wa kwanza kisha akaondoka anaandikiwa kuswali usiku mzima?

Swali: Baadhi ya misikiti kama mfano wa msikiti mtukufu wa Makkah wanaswali kwa Tasliym kumi ambapo kila baada ya Tasliym tano anaziswali imamu. Nikiswali nyuma ya imamu wa kwanza kisha nikaondoka naandikiwa kuwa nimeswali usiku mzima au ni lazima nikamilishe?

Jibu: Ni lazima ukamilishe. Hilo ni kwa sababu imamu wa pili ni naibu wa imamu wa kwanza. Dalili juu ya hili ni kwamba Witr inakuwa pamoja na yule imamu wa pili. Ukweli wa mambo ni kwamba yule wa kwanza hakukamilisha swalah yake. Bali ameswali baadhi ya swalah na akaikamilisha yule mwengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1601
  • Imechapishwa: 19/03/2020