Mtu akiona najisi ndani ya swalah afanye nini?

Swali: Mtu akiona najisi wakati yuko anaswali aendelee na swalah yake au ajaribu kuiondoa najisi hii…

Jibu: Ikiwa anaweza kuondoa nguo ilio na najisi na aswali kwenye nguo nyingine, aivue na kukamilisha swalah yake. Hivo ndivyo alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipokuwa anaswali kwenye viatu vyake na akavivua ndani ya swalah na Maswahabah nao (Radhiya Allaahu ´anhum) wakavua viatu vyao wakimuiga (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pindi alipotoa Tasliym akawauliza ni kwa nini walifanya vile ambapo wakajibu kuwa ni kwa sababu walimuona yeye anavua viatu vyake. Ndipo akawaambia kuwa Jibriyl ndiye alimjuza ya kwamba vina uchafu. Ni dalili yenye kuonesha kuwa mtu akiweza kuvua nguo ilio na najisi ndani ya swalah na akakamilisha swalah yake ni sahihi. Ama akishindwa kuivua nguo hii, anatakiwa kukata swalah yake na aondoshe najisi kisha baada ya hapo aianze swalah yake mwanzo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%208%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017