Mtu akinuia kubaki katika mji zaidi ya siku nne aswali kikamilifu au afupishe?

Swali 337: Mtu akinuia kubaki katika mji zaidi ya siku nne aswali kikamilifu au afupishe?

Jibu: Siku nne hazina mafungamano na hali ya ukazi au safari. Ukazi na safari ni jambo lililofungamana na nia ya yule mwenye kufanya ´ibaadah na hali yake. Yule anayekwenda katika mji kwa mfano kwa ajili ya kufanya biashara na akakadiria biashara hiyo itamchukua siku nne, basi mtu huyo hawi mkazi. Kwa sababu bado ni mwenye kuendelea msafiri kutokana na nia yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 127
  • Imechapishwa: 05/09/2019