Mtu afanye nini ikiwa alimpa zawadi ya TV rafiki yake?

Swali: Kitambo nilikuwa na king´amuzi/dishi na nikaipeana zawadi kwa mmoja katika ndugu zangu. Hivi sasa baada ya Allaah kunitunuku uongofu nimeona niivunje. Nifanye vipi pamoja na kuzingatia kwamba siwezi kumuomba nayo kwa sababu anaweza kunifahamu makosa na kunidhania vibaya na kufikiria kwamba sitaki kumpa nayo au kwamba nimejirudi katika kumpa zawadi?

Jibu: Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye amemtunuku huyu uongofu. Aende kwa yule aliyempa zawadi na amuulize kama anaitumia katika mambo ya haramu – kama wanavyofanya watu mara nyingi – au anaitumia katika taarifa ya khabari tu? Ikiwa ni hili la pili na mtu huyo akawa ni mwaminifu hakuna neno. Ikiwa ni hilo la kwanza ya kwamba anatazama kupitia dishi hiyo kila kinachorushwa, basi amwambie mtu huyo kwamba mimi nimemwagiza ampokonye nayo na aivunje mbele ya huyo mtu uliyempa zawadi. Kwa kufanya hivo hayo mashaka kwa huyo mtu aliyempa zawadi yatamwondoka na atakinaika – Allaah (´Azza wa Jall) akitaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (77) http://binothaimeen.net/content/1770
  • Imechapishwa: 16/09/2020