Mtoto kuuza vitu vya baba yake bila yeye kujua


Swali: Mimi ni mwanafunzi ninayesoma chuo kikuu cha Shari´ah. Nahitajia vitabu vingi kama inavojulikana. Baba yangu ana maktabah ambayo kwa hivi sasa haitumii kwa sababu ya kushughulishwa na kazi za idara. Pamoja na kuzingatia kwamba maktabah yake yote haina vitabu vya dini. Ina vitabu vya elimu mbalimbali visivyohusiana na yale ninayoyasoma. Je, inafaa kwangu kuchukua vitabu na kuviuza ili nipate kununua vitabu ninavyohitajia bila ya idhini yake wala yeye kutambua?

Jibu: Haifai kwa mtoto kuchukua katika mali hii. Haifai kwake kuchukua kutoka katika pesa za baba yake isipokuwa kwa yeye kujua. Lakini amuombe idhini baba yake au amuombe ampe pesa au amruhusu kuuza vitabu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 06/07/2019