Mtoto kupuliziwa roho na kuandikiwa matendo yake tumboni   

Mtoto kupuliziwa roho ni jambo limefungamanishwa na kuandikiwa ´amali zake au ni baada ya siku mia moja na ishirini? Wanachuoni wametofautiana juu ya hili:

1- Kuna jopo la wanachuoni lililosema ya kwamba kupuliziwa kwa roho hakukuwi isipokuwa baada ya siku mia moja na ishirini. Kwa sababu amesema (´alayhis-Salaam):

“… halafu hupelekwa Malaika anayempulizia roho.”

Kwa ajili hii kuna jopo la Maswahabah, na maoni haya yamechaguliwa pia na Imaam Ahmad na wengineo, ya kwamba mtoto hupuliziwa roho katika zile siku kumi moja kwa moja baada ya kueneza miezi mine.

2- Wanachuoni wengine wamesema kuwa anapuliziwa roho baada ya kutimiza miezi mine na siku kumi kutokana na mapokezi yaliyopokelewa kutoka kwa Maswahabah juu ya hilo.

3- Wengine wakasema kuwa kupuliziwa kwa roho hapa kumeambatanishwa na kumeoanishwa na uandikiwaji wake. Amesema (´alayhis-Salaam):

“… halafu hupelekwa Malaika anayempulizia roho na anaamrishwa mambo manne.”

Kuamrishwa mambo mane kukaambatanishwa na kupuliziwa kwa roho. Kutokana na Hadiyth zingine tunajua kuwa mambo haya huandikwa kabla ya hapo na wakati Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hazigongani bali zinaafikiana kwa kuwa haki haiigongi haki nyingine. Zote zinasadikishana. Wamesema kuwa linatokana na aghalabu. Lakini hata hivyo anaweza kupuliziwa roho na kuanza kufanya harakati kabla ya hapo. Kwa kuwa kupuliziwa roho kumeambatanishwa na uandikaji. Hadiyth zimeonyesha kuwa kinachotangulia ni uandikaji. Hilo lina maana ya kwamba kupuliziwa kwa roho kuna uwezekano kukawa ndani ya siku mia moja na ishirini.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 107-108
  • Imechapishwa: 17/05/2020