Swali: Bwana huyu amepewa mtihani watoto wake hawaendi kuswali msikitini lakini wanaswali nyumbani kwao. Wamemchokesha kuwaongoza na kuwanasihi mpaka amefikia kuwapiga. Ni lipi la wajibu juu yake?

Jibu: Hili ndio la wajibu kuwachapa. Akishindwa basi aende kuwashtaki mamlaka husika ikiwa ipo nchini mwake au baraza lenye nguvu zaidi.

Swali: Mmoja wao amepewa mtihani msichana wake haswali kabisa.

Jibu: Vivyo hivyo amchape mpaka asimame sawasawa. Akimtia adabu atanyooka – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21685/حكم-تاديب-الابناء-لتقصيرهم-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 16/09/2022