Mtoto aliyefikisha miaka 15 anashindwa kufunga mpaka maghrib

Swali: Ni ipi hukumu kwa mtu aliyefikisha miaka 15 kwa hoja ya kuchoka sana na kutoweza kutimiza funga yake siku hii? Ikiwa atalipa inafaa kwake kulipa baada ya kupita Ramadhaan nyingine?

Jibu: Ni haramu kwa mtu ambaye inawajibika kwake kufanya ´ibaadah – المكلف – kuacha kufunga. Mtu huyo ni yule ambaye ni muislamu, mwenye akili, ambaye kishabaleghe, mkazi na mwenye afya njema. Swawm ikimuwia ngumu na akalazimika kula – kama anavyolazimika mtu wakati mwingine kula nyamafu – itakuwa inajuzu kwake kula kwa kiasi cha kujiondolea maangamivu kisha ajizuie siku iliyobaki na kuilipa siku nyingine baada ya Ramadhaan.  Akichelewesha mpaka ikaingia Ramadhaan nyingine pasi na udhuru basi atatakiwa kulipa na kulisha kwa kila siku moja masikini.

Ambaye kishatimiza miaka 15 kamilifu kishabaleghe. Kadhalika yule mwenye kushusha manii kwa matamanio ima wakati wa kuota au wakati mwingine. Vivyo hivyo yule mwenye kuota nywele sehemu ya siri. Kunaongezeka kwa mwanamke kitu cha nne ambacho ni kupata hedhi.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/237)
  • Imechapishwa: 10/06/2017