Mtoto afanye nini kwa baba ambaye ana uwezo na hataki kumuoza?

Mtu akiwa na watoto wanaohitaji kuoa na yeye akawa ni tajiri ni wajibu kuwaoza kama ilivyo wajibu kuwaangalia kwa chakula, kinywaji, mavazi na makazi. Ni wajibu awaoze. Asipofanya hivo na watoto wakaweza kuchukua kitu kidogo katika mali yake – hata kama watafanya hivo kwa kujificha – ili waweze kuwaoa wana haki ya kufanya hivo. Ni kama jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyompa idhini Hind bint ´Utbah alipomshtaki mume wake ambaye alikuwa hampi yeye na watoto wake matumizi ya kuwatosha, akamwambia:

“Chukua kiasi kinachokutosheleza wewe na wanao kwa wema.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (22)
  • Imechapishwa: 30/12/2018