Swali: Nataraji kuwekewa wazi jambo hili kwa vile linazungumziwa kwa wingi; hukumu ya uchafuchafu na manjano yanayomtoka mwanamke baada ya kukatika damu yake? Ni lini kunakuwa kutwahirika kwa mwanamke? Ni lazima atokwe na al-Qaswah al-Baydhwaa´ [mtiririko mweupe]?

Jibu: Masuala haya wanachuoni wametofautiana kwayo. Maoni niliyoona kuwa na nguvu kipindi cha mwisho ni kwamba uchafuchafu wala manjano hayazingatiwi isipokuwa yale yaliyo katikati ya hedhi[1]. Kwa mfano mwanamke amezowea kupata ada yake ya mwezi siku tano. Ile siku tano akaona uchafuchafu au manjano. Katika hali hii tunasema kuwa inafuata hedhi. Upande mwingine mwanamke amejiwa na uchafuchafu na manjano kabla ya kutokwa na damu. Uchafuchafu au manjano havizingatiwi. Mwanamke mwingine ametwahirika na hedhi na damu imekatika. Lakini hata hivyo kukabaki uchafuchafu au manjano. Pia havizingatiwi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/amesafika-na-hedhi-lakini-haoni-mtiririko-mweupe-ukitoka/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (73) http://binothaimeen.net/content/1705
  • Imechapishwa: 14/04/2020