Ahmad al-Ghumaariy amesema:

“Tambua kwamba Hadiyth zilizopokelewa juu ya watokaji ni zenye kufanana na Hadiyth za Khawaarij. Hata kama wote ni wenye kutoka katika dini (خوارج عن الدين) na wote ni mijibwa ya Motoni, kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), pamoja na hivo wamegawanyika mafungu mawili:

1 – Fungu la kwanza wanatambulika kwa jina hili. Wamesifiwa kuwa ni wenye kujikakama na kuchupa mpaka katika dini na kwamba mmoja wetu atazidharau swalah na swawm zake ukilinganisha na swalah na swawm zao.

2 – Fungu la pili ni wale wapotofu wa sasa (ملاحدة العصر). Wamesifiwa kuwa wapumbavu na vijana na kwamba alama zao ni kunyoa upara.

Pindi kulipozuka pembe ya shaytwaan huko Najd mwishoni mwa karne ya kumi na fitina yake ikaenea, basi wanachuoni wote walikuwa wakizitumia Hadiyth hizi juu yake na wafuasi wake, kwa sababu kulikuwa hakujazuka aina ya Khawaarij hawa hapo kabla.”[1]

Nne: Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab aliishi na kuhuisha dini huko Najd mwishoni mwa karne ya kumi na mbili na si mwanzoni mwa karne ya kumi na moja kama anavodai mtunzi wa kitabu.

Tano: Miongoni mwa mambo yanayojulisha uelewa wa kiharibifu wa mtunzi ni kule kumtuhumu Shaykh ambaye ni muhuishaji wa dini na kueneza Sunnah kwamba ni kueneza fitina. Huu ndio mtindo wa Ahl-ul-Bid´ah ambao mioyo yao iko chini-juu. Wakawa wanaona haki kuwa ni batili na batili kuwa ni haki. Allaah atulinde kutokamana na ufahamu wa upofu.

[1] Mutaabaqat-ul-Ikhtara´aat al-´Asriyyah, uk. 76

  • Mhusika: ´Allaamah Hamuud bin ´Abdillaah at-Tuwayjiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iydhwaah-ul-Mahajjah, uk. 139-140
  • Imechapishwa: 09/07/2020