Suruuriyyuun, ni mamoja walioko Saudi Arabia au Yemen, wanawachezea shere wanachuoni na kuwatia ujingani. Hili linatolewa dalili na gezeti la ”as-Sunnah”. Mimi hapo kitambo nilikuwa nikisifia gazeti la ”as-Sunnah” na ”al-Bayaan”. Lakini hata hivyo wanawachezea shere wanachuoni na kuwatuhumu kwamba hawajui chochote juu ya mambo ya kisasa tofauti na wale chipukizi  ambao wao wanatambua mambo ya kisasa.

Miongoni mwa alama za Hizbiyyuun ni kwamba huwachezea shere wanachuoni na kuwafanya watu wakakimbia mbali kuketi chini pamoja na wanachuoni. Hili ni jambo linalowafurahisha maadui wa Uislamu bali na mashaytwaan.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=16
  • Imechapishwa: 05/12/2020