Mtihani wa mali ni mkubwa kuliko mtihani wa watoto

Swali: Ni ipi hekima ya mali kutangulizwa kutajwa kabla ya watoto ndani ya Qur-aan tukufu ingawa baba huona watoto ni wenye maana zaidi kuliko mali?

Jibu: Mali husaidia kufikia matamanio yaliyoharamishwa tofauti na watoto. Mtu anaweza kupewa mtihani kwao na akamuasi Allaah kwa ajili yao. Mtihani wa mali ni kubwa na khatari zaidi. Kwa ajili hiyo ameanza (Subhaanah) kutaja mali kabla ya watoto. Mfano ni katika maneno Yake (Ta´ala):

وَمَا أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُم بِالَّتِي تُقَرِّبُكُمْ عِندَنَا زُلْفَىٰ إِلَّا مَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ جَزَاءُ الضِّعْفِ بِمَا عَمِلُوا وَهُمْ فِي الْغُرُفَاتِ آمِنُونَ

“Na hazikuwa mali zenu na wala watoto wenu ambavyo vitakukurubisheni Kwetu muwe karibu isipokuwa yule aliyeamini na akafanya matendo mema, basi hao watapata malipo maradufu kwa yale waliyoyatenda – nao watakuwa katika maghorofa hali ya kuwa ni wenye amani.”[1]

إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ ۚ وَاللَّـهُ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ

”Hakika si venginevyo mali zenu na watoto wenu ni jaribio; na kwa Allaah kuna ujira mkubwa.”[2]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ

“Enyi walioamini! Zisikushughulisheni mali zenu na wala watoto wenu mkaacha kumtaja Allaah. Na yeyote atakayefanya hivyo, basi hao ndio waliokhasirika.”[3]

[1] 34:37

[2] 64:15

[3] 63:09

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/379)
  • Imechapishwa: 01/08/2021