Mti wa imani mioyoni


Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah tano, ijumaa hadi ijumaa nyingine, Ramadhaan hadi Ramadhan nyingine, ni kifutio cha yaliyoko kati yake muda wa kuwa kunaepukwa madhambi makubwa.”[1]

Hadiyth hii inajulisha fadhilah za Allaah na ukubwa wa ukarimu Wake kwa kufadhilisha ´ibaadah hizi tatu kuu na kwamba zina nafasi ya juu mbele ya Allaah. Moja katika faida zake kubwa ni kwamba Allaah amezifanya kwamba ni zenye kukamilish dini na Uislamu wa mja, zinailea imani na kumwagilia maji mti wake. Allaah amepanda mti wa iman kwenye mioyo ya waumini na inakuwa kutegemea na imani yao. Kutokana na upole na fadhilah Zake amekadiria mambo ya wajibu na yaliyopendekezwa ili mti huu uweze kutiwa maji na kuukuza pamoja na kuulinda na magonjwa mpaka uweze kukamilika na mwishowe utoe matunda yake. Madhambi magonjwa yake ni makubwa na ni jambo linatambulika vyema kwamba yanaipunguza imani.

[1] Muslim.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bahjat-ul-Abraar, uk. 73
  • Imechapishwa: 22/02/2021