Mti kuota kwenye kaburi ni dalili ya wema wa maiti?

Swali: Sisi kwetu watu wasiokuwa na elimu huweka kwenye kaburi la maiti mti. Halafu akishazikwa na baada ya kupita muda fulani tangu siku ile aliyozikwa kuna miti ambayo hukauka na mingine humea mpaka inayafunika baadhi ya makaburi. Wakasema hawa ndio mawalii wa Allaah kwa kuwa mti umemea kwenye makaburi yao. Haya ni sahihi? Ni zipi nasaha zako?

Jibu: Si sahihi. Haya ni ukhurafi ambao Allaah hakuteremsha dalili yoyote juu yake. Kuota mti juu ya kaburi sio dalili ya kwamba mtu ni walii. Miti huota hata kwenye makaburi ya makafiri. Miti huota kwa udongo na mvua na haina uhusiano wowote na yule maiti. Haya ni katika ukhurafi na batili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (03) http://alfawzan.af.org.sa/node/2046
  • Imechapishwa: 13/10/2016