Mtazamo wa wanachuoni wengi juu ya manukato yenye alcohol

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia manukato yaliyo na alcohol? Ni najisi? Je, ni sahihi kuswali nayo au hapana?

Jibu: Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa ni najisi. Kujengea juu ya hili inatakikana kwa mtu kuosha nguo yake. Baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa sio najisi. Pombe hailazimishi kupatikana kwa najisi. Lakini hata hivyo wanachuoni wengi wanaonelea kuwa ni najisi ikiwa inalewesha.

Inatakikana kwa mtu kuchukua lililo salama na asijitie manukato yaliyo na alcohol. Kwa sababu uhakika wa mambo haya sio manukato. Manukato yanajulikana kama misiki. Ni kama udi, maji ya mauwa n.k. Ikiwa kuna asilimia kubwa ya alcohol basi inatakikana kwa mtu ajiepushe nayo kwa ajili ya usalama. Kwa sababu wanachuoni wengi wanaonelea kuwa ni najisi. Ama ikiwa kuna asilimia ndogo ya alcohol, basi ni yenye kusamehewe. Uhalisia wa mambo ni yenye kutumika kutibu madonda na hayatumiwi kama manukato.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 01/03/2018