al-Khaliyliy amesema:

“Ni maneno yaliyoteremshwa kwa herufi na maneno yake kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… “

Hakusema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah yaliyoanza Kwake pasi na namna kwa kuwa anapinga Allaah kuwa na sifa ya kuzungumza. Halafu baada ya hapo akaweka wazi zaidi ya kwamba Qur-aan imeumbwa kama viumbe wengine wote akiilinganisha na kuumbwa kwa mwanaadamu, mnyama, mbingu, ardhi na kadhalika. Amesema:

“Allaah aliipulizia Qur-aan kutoka katika roho iliyofichikana kama ilivyo kwa mwanaadamu ambaye Allaah (Ta´ala) amemuumba kutokana na udongo.”[1]

Hivi ndivyo anavyosema.

Amesema tena:

“Kuhusu sisi Ibaadhiyyah tunaosema kuwa Qur-aan imeumbwa na wale wanaoonelea maoni yetu katika Mu´tazilah na wengineo… “[2]

Ni jambo linalojulikana mbali na Mu´tazilah na Ibaadhiyyah wanaoonelea kuwa Qur-aan imeumbwa ni Jahmiyyah ambao ndio msingi wa kuzua upotevu huu. Vilevile Imaamiyyah katika Raafidhwah na wale waliofuata mapito yao katika mlango wa majina na sifa za Allaah. Hapa amethibitisha kuwa Ibaadhiyyah ndio msingi waliozusha Bid´ah hii na kwamba Mu´tazilah wakafuatia…

[1] Uk. 101

[2] Uk. 125

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 157-158
  • Imechapishwa: 14/01/2017