Mtazamo wa Ashaa´irah juu ya ujuu na kulingana kwa Allaah


Ashaa´irah hawamthibitishii ujuu wa Mola wala kulingana Kwake juu ya ´Arshi. Wanawaita wale wenye kuthibitisha ujuu na kulingana Mujassimah na Mushabbihah. Hili ni tofauti na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wanathibitisha ujuu na kulingana kwa Allaah, kitu ambacho Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amekielezea Mwenyewe na vilevile Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya yanatakiwa kuthibitishwa bila ya kuiwekea namna wala ukanushaji. Salaf wengi wamemkafirisha yule asiyethibitisha sifa ya ujuu na kulingana.

Ashaa´irah wanaafikiana na Jahmiyyah kwa kukanusha sifa hii. Lakini Jahmiyyah wanasema kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko kila mahali na ndio maana wakaitwa Huluuliyyah, upande mwingine Ashaa´irah wanasema kwamba Allaah alikuwepo wakati hakukuwepo sehemu yoyote na kwamba Yuko katika hali hiyo hiyo aliyokuwepo kabla ya kuumba sehemu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan Abaa Butwayn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Rasaa-il wal-Masaa-il an-Najdiyyah (2/176)
  • Imechapishwa: 09/04/2017